WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Geita Gold wamewashukuru mashabiki kwa sapoti yao licha ya kupoteza mchezo wa kwanza kimataifa kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Hilal Al Sahil.

Kocha Mkuu wa Geita Gold, Felix Minziro aliongoza kikosi hicho kwenye mchezo huo na sasa ni mahesabu kuelekea mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 17,2022.

Geita Gold, Geita Gold Wapania Makubwa Kimataifa, Meridianbet

Kwa mujibu wa Mathias Wandiba, kocha msaidizi wa Geita Gold aliweka wazi kuwa kila mmoja anakazi kubwa ya kufanya kutafuta ushindi wa timu.

“Bado kazi ipo na kila mchezaji anapenda kupata matokeo, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi tuna amini kuwa tutafikia malengo yetu,” amesema.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa