MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla leo ametembelea Uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju.

Makala ameruhusu uongozi wa Klabu ya Simba kuendelea na mradi wa ujenzi wa ukuta kuzunguka eneo hilo ukiwa ni mpango kazi wa ujenzi wa viwanja vya michezo.

Simba, Amos Makalla Atembelea Mo Simba Arena, Meridianbet

Aidha kiongozi huyo amewaagiza watu waliovamia eneo hilo kuhama ndani ya siku 60.
Pia mkandarasi wa ujenzi wa ukuta huo kwenye uwanja wa Mo Simba Arena tayari amefika eneo la kazi kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kuwekeza katika eneo la uwanja kwa kuwa na viwanja vya nyasi bandia na asilia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa