Mshambuliaji wa Tottenham Hot Spurs Harry Kane amefunga mabao 19 katika mechi 18 alizocheza dhidi ya Leicester City toka timu hiyo inayoongozwa na Brendan Rodgers ipanda daraja.

 

Kane: Mabao 19 Kwenye Mechi 18 Dhidi ya Leicester City

Kane amekuwa ni katili anapokuwa mbele ya goli hivyo ni mchezaji anayetakiwa kuchungwa sana akiwa ndani ya 18. Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa anataka kuondoka klabuni hapo na atimkie Manchester City na baadae akaamua kusalia klabuni hapo.

Amekuwa akihusishwa na vilabu mbalimbali ikiwemo Bayern Munich ya Ujerumani huku klabu hiyo ikimtaka kwa hali na mali mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Uingereza huku tetesi zikisema kuwa atasajiliwa na miamba hao dirisha dogo Januari. Kane amekuwa na mwendelezo mzuri wa ufungaji wa mabao.

 

Kane: Mabao 19 Kwenye Mechi 18 Dhidi ya Leicester City

Mchezaji huyo mpaka sasa katika mechi sita za Spurs alizocheza amepachika mabao matano huku akishikilia nafasi ya 4 katika wafungaji bora wa EPL. Hivyo kama atafunga bao leo au mabao atakuwa amejiongezea mabao huku akiwa na mabao mengi kuliko mechi alizocheza na Leicester City ambao wana hali mbali kwani wako mkiani.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa