Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Rally Bwalya, amesema baada ya kukosa nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa sasa ni wakati wa kufanya hivyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Kiungo huyo ameweka wazi malengo ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi ni kuhakikisha Simba SC wanaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa kuitoa Red Arrows.
Bwalya amesema mchezo wa kwanza dhidi Wazambia hao utakuwa mgumu kwa sababu wapinzani nao watataka kutafuta matokeo ugenini ili kurahisisha mechi ya marudiano lakini wapo tayari kuwakabili katika mechi zote mbili.
“Red Arrows si timu mbaya ndiyo maana imefika hatua hii na hatutaidharau, tutaingia uwanjani kupambana kutafuta ushindi tukijua tupo nyumbani. Tutaingia uwanjani kuhakikisha tunapambana kutafuta ushindi.
“Tulikuwa na nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa lakini ikashindikana, sasa tumepata tena nafasi ya kufanya hivyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika tutahakikisha inawezekana,” amesema Bwalya.

Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.


