Wanayopitia Manchester United kwenye soka, kinafanana na wanachopitia LA Lakers kwenye NBA msimu huu.
Lakers wamejikuta wakiambulia kipigo cha 5 kati ya michezo 7 waliyocheza hivi karibuni. Hali sio shwari pale Staple Centre msimu huu. Matokeo mabaya na uwepo wa majeruhi, ni miongoni mwa changamoto wanazopitia.
Wakiwa nyumbani dhidi ya Sacramento Kings, vigogo wa Los Angeles wameambulia kipigo cha pointi 141-137. LeBron James, Russell Westbrook na Anthony Davis kwa pamoja wamepachika pointi 82. Watamalizaje msimu huu?

Kwingineko kwenye NBA, Stephen Curry ameiongoza Golden State Warriors kupata ushindi wa 10 wakiwa nyumbani. Warriors wameshinda kwa pointi 118-103 dhidi ya Portland Trail Blazers. Giannis Antetokounmpo ameiongoza Milwaukee Bucks kwenye ushindi wa pointi 120-109 dhidi ya Denver Nuggets.
Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.