Chelsea Vitani na Liverpool kwa Lavia

Klabu ya Chelsea imeingia vitani na klabu ya Liverpool katika kumuwania kiungo wa klabu ya Southampton raia wa kimataifa wa Ubelgiji Romeo Lavia.

Chelsea imetaarifiwa kupeleka kiasi cha paundi milioni 48 ambazo bonasi zitafata baadae, Lakini klabu ya Southampton inaarifiwa kuhitaji kiasi cha puandi milioni 50 kwa kiungo Romeo Lavia.chelseaLiverpool wamepeleka ofa kwa klabu ya Southampton mara kadhaa na zimekua zikipigwa chini ikiwa ni kutokana na kutokidhi mahitaji ya klabu hiyo, Hivo ni wazi Liverpool wanaweza kumkosa mchezaji huyo kama matajiri wa London watapanda dau zaidi.

Klabu ya Southampton wao walipokea ofa ya mwisho ya Liverpool ilikua ni paundi milioni 45 ikiwa ni pungufu na ambayo The Blues walipeleka ya paundi milioni 48 mpaka sasa klabu hiyo chini ya tajiri Toddy Boehly wanaonekana wanaweza kumchukua mchezaji huyo.chelseaChelsea inaelezwa imeamua kuhamia kwa kiungo Romeo Lavia baada ya klabu ya Brighton kugoma kuchukua kiasi cha Euro milioni 80,Jambo lililowafanya klabu hiyo kutoka jijini London kutafuta mbadala mwingine na Romeo Lavia ndio ameonekana mtu sahihi.

Acha ujumbe