'Chirwa ni Asset' - Azam

Azam FC wamesema sababu ya kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja Obrey Chirwa.

Afisa Habari wa klabu Thabith Zakaria, amesema wamefikia makubaliano ya kumuongezea mkataba baada ya kiwango chake kuishauri klabu.

Chirwa ambaye hivi juzi amesaini mkabata wa mwaka mmoja ambaye utamfanya kusalia na wanalamba lamba kwa mwaka 2020/21 baada ya klabu kusema yeye ni ‘asset’.

“Tumefikia makubaliano ya kuongeza mkataba kwa sababu bado ni mchezaji kwenye kikosi na huduma yake bao tunaihitaji msimu ujao,” amenukuliwa Zakaria.

“Ni mchezaji mzuri na klabu inafuraha kuwa nae.”

Zakaria ameongeza kuwa mazungumzo na Chirwa yalienda vizuri kwasababu mchezaji hakukwenda kwao Zimbabwe kwasababu ya janga la Corona.

Hata hivyo, Zakaria amesema mustakabali wa mshambuliaji Donald Ngoma bado haujajulikana kwani bado pande hizo mbili hazijakutana kuzungumzia kuhusu kuongeza mkatba mpya.

Chirwa alijiunga na Azama 2018 akitokea Yanga lakini majiraha ya kila mara yamefanya asicheze kila mara, pamoja na kung’aa akiwa na Yanga.

Azam, mara mwisho kushinda taji la VPL 2014, wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 24 na michezo 28.

Acha ujumbe