Jioni ya Tarehe 30 Disemba mwaka 1975 katika viunga vya Cypress jijini Califonia nchini Marekani anazaliwa kijanamwenye bahati na aliyjijengea heshima kubwa kwa taifa lake na dunia ya wanamichezo wa mchezo wa Golf. Eldrick Tont Woods maarufu kama Tiger Woods hili jina laweza kua sigeni sana kwa wanaofatilia michezo, hususan mchezo unaohisiwa kua unachezwa na watu wenye vipato vya juu sana Duniani wa Golf.

Woods akiwa na miaka 6 uwezo wake ulianza kutambulika na jamii ya wamarekani ambapo akiwa tu na umri huo alisha anza kuonekana kwenye televisheni akionesha uwezo wake wa kucheza Golf, Mwalimu na mshawishi mkubwa wa Tiger Woods kuingia kwenye mchezo wa Golf ni baba yake ambae alikua ni mwanajeshi mstaafu wa jeshi la Marekani, na ndie aliyempa jina la Tiger kijana wake huyo akimuenzi rafiki yake aliyefariki Jeshini.
Akiwa mwaka wa kwanza tu Chuoni tayari akawa mcheza gofu tasmi mwaka 1996 akiwa na miaka 20 tu, Mwishoni mwa mwezi wa nne mwaka 1997 akawa tayari ameshinda mataji matatu ya PGA (Professional Golf Association) , na kwa mara ya kwanza mwezi juni mwaka 1997 anavunja rekodi ya kua Mmarekani mwenye Asili ya Africa wa kwanza kuwa namba moja kwenye Ngazi za wacheza gofu bora duniani, Vyote vikitokea chini ya mwaka mmoja tangu aanze kucheza Gofu kimataifa.

Kwa mwaka huo wa 1997 pekee Woods aliweka rekodi ambazo hazija wahi kufikiwa na baadhi ya wacheza gofu wakubwa walio mfuata baada ya kipindi chake, katika kuonekana kwake kwa mara ya kwanza kwenye British Open Woods alifikia rekodi ya kupata point 64. Na miaka iliyofata ikawa ya mafanikio makubwa sana kwa mtaalamu huyo wa kulenga mashimo kwa vipira vidogo vyeupe.
Sylvester
Bonge la nguli katika Golf kumbe alianza kua shujaa toka mtoto.Asante kwa habari nzur #meridianbettz