Arsenal imeripotiwa kujiondoa kwenye mazungumzo ya mkataba mpya kati yao na nahodha Pierre-Emerick Aubameryang. Baba mzazi wa mchezaji huyo awali alidokeza kuwa mchezaji huyo anaweza kusaini mkataba mpya huko Emirates lakini kwa mujibu wa ‘TheExpress’, Arsenal sasa imejiondoa kwenye mazungumzo na Inter Milan inaripotiwa kuwa inaongoza mbio za kunasa saini yake.
Katika ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram, Aubameyang aliweka picha ya mtoto wake akisaini mkataba wake wa kwanza na Arsenal mnamo 2018, pamoja na maelezo: “Unajua nini cha kufanya bro @aubameyang97.”
Inaaminika kuwa Mazungumzo kati ya mchezaji na klabu yamekuwa yakiendelea kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anaonekana kutaka kuongezwa kwa mshahara wake wa sasa wa pauni 200,000 kwa wiki lakini inasemekana kwamba madai yake yamekuwa juu sana kwa Arsenal.
Aubameyang anahitaji pauni 300,000 kwa wiki, mshahara karibia na ule wa Mesut Ozil wa pauni 350,000-kwa wiki, na Arsenal inasemekana haikuwa na nia ya kumpa mchezaji mwingine kiasi hicho kwani wanataka kupunguza bajeti ya mishahara kwenye timu.
Kando na Inter Milan, nahodha huyo wa Gabon amehusishwa na kuhamia Manchester United, Barcelona, Real Madrid na Chelsea.
Aubameyang amefunga mabao 17 ya Ligi Kuu msimu huu na anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake.
farida ahmadi
Asante kwa taarifa