Timu za Serie A zinatarajia kurejea dimbani na kuanza mazoezi binafsi mapema mwezi Mei, kabla ya kuanza mazoezi ya Jumla ya timu nchini humo.
Kutokana na tangazo la Waziri Mkuu wa Italia juu ya hatua za awali juu ya kufungwa kwa nchi na shughuli zingine, kuna matumaini kuwa vilabu vitakuwa vinaweza kufanya mazoezi binafsi ya wachezaji kuanzia tarehe 5 Mei
Kuna matumaini makubwa kuwa mechi za Ligi ya Serie A zinaweza kuendelea kuanzia tarehe 27 Mei hadi Tarehe 2 Juni wakati msimu ukiwa unatarajiwa kufika Tamati mwezi Agosti.
Hata hivyo, licha ya matumaini haya ambayo yanatokana na maendeleo ya jitihada za kumbambana na janga la Corona, bado hakuna tangazo rasmi kuwa Ligi itaendelea kuanzia tarehe ngapi. Waendeshaji wa ligi wanatarahia kusoma upepo wa mapambano na kufuata maelekezo ya serikali.
Jumapili Italia iliripoti idadi ya watu 260 waliofariki kwa Corona, ikiwa ni idadi ndogo zaidi kuripotiwa tangu tangu tarehe 14 Machi.
Kwa mujibu wa waziri mkuu, wachezaji watakuwa wanaweza kufanya mazoezi binafsi kuanzia tarehe 4 Mei, na kwa makundi kuanzia tarehe 18 Mei. Baada ya hapo kutafanyika tathmini kuhusu uwezekano wa kumalizia msimu.
Waziri amesisitiza kuwa Italia wanapenda michezo lakini hawahitaji kuwaweka wachezaji matatani hivyo ni muhimu wao kuwa makini zaidi wanapotaka kufanya maamuzi ya aina hii.


TATU
IRUDI TULIKUWA TUNAISUBILI KWA HAMU
farida ahmadi
Habari nzuri Sana kwetu mashabiki