Scott McTominay: Nilistahili Kusalia United

Scott McTominay ameweka wazi kuwa kulikuwa na uwezekano wa yeye kuondoka klabuni Manchester United kwa mkopo lakini yeye alitaka kusalia Manchester United akiamini ndipo alipoikuwa anatakiwa kuwepo.

Mara nyingi klabu zimekuwa zikiwatoa wachezaji ambao wana uwezo lakini wanapata mda mchache wa kucheza ili waende wakacheze vilabu vingine kwa mkopo. Huko wapate angalau mda zaidi wa kucheza na kujiboresha.

McTominay alikuwa ameandaliwa kuondoka klabuni hapo wakati fulani akiwa anatokea Akademi ya klabu, lakini aliamua kubaki.

Kiungo huyu, raia wa Scotland alicheza mechi yake ya kwanza akiwa chini ya Jose Mourinho walipofungwa bao 2-0 Mei 2017, hata baada ya meneja kuondoka klabuni hapo ameendelea kufanya vyema chini ya Ole Gunnar.

Maneno ya Scott McTominay:

“Ilikuwa ni kama mwaka mmoja uliopita, ni kama kulikuwa na uwezekano wa kuondoka kwa mkopo lakini mtu mwingine akaondoka.”

“Unasikia stori nyingi sana kuhusu vijana kuchukuliwa kwa mkopo, nja mambo mengine tofauti kama hayo. Wakati wote nilikuwa nikifikiri hili kichwani mwangu kuwa siyo kitu nilichokuwa nakihitaji. Nataka kujionesha hapa kwanza, na kama ikishindikana hapa, ndiyo unaondoka kwenda sehemu nyingine.”

3 Komentara

    Glory Glory Man United

    Jibu

    Baki tu.

    Jibu

    Mc tominay ni moto united umepamudu

    Jibu

Acha ujumbe