Kocha mkuu wa klabu ya Tottenham Antonio Conte amewajibu watu wanaomkosoa kufuatia kipigo cha Tottenham dhidi ya Arsenal akisema kuwa, “Naweza kufundisha soka kwa watu wengi”
Spurs walipoteza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu siku ya Jumamosi kwa mabao 3-1 na leo hii wanajiandaa kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Eintratch Frankfurt baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Sporting.
Wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi Jumatatu, Conte alijibu shutuma zake, akisisitiza kwamba anaweza kufundisha soka kwa wengi na kudai ushindi wake nchini Italia na Uingereza.
Spurs wameshinda mara moja na kupoteza mara moja katika mechi mbili za kwanza za Ligi ya Mabingwa msimu huu. Na Conte mkataba wake unatarajiwa kumalizika mnamo Juni 2023.