Nyota wa Juventus Angel Di Maria anayecheza katika nafasi ya winga amekanusha ripoti kwamba yeye na mchezaji mwenzake Leandro Paredes wameitaka klabu yao kutocheza mechi ya Novemba kabla ya Kombe la Dunia.

 

Di Maria Akanusha Habari za Uongo.

Ripoti nchini Argentina zinasema kwamba AFA inatarajia wachezaji wao kutohusika katika michezo ya mwisho ya ligi mwakani kabla ya Kombe la Dunia.

Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza Novemba 20,  na Wamarekani wa Kusini watacheza kwa mara ya kwanza siku mbili baadaye dhidi ya Saudi Arabia.

Paredes na Di Maria wanatarajiwa kuingia kwenye kikosi cha Argentina kitakachocheza Qatar 2022, lakini El Fideo amekanusha kuwa watawaomba Juventus wasihusishwe kwenye mchezo wa mwisho kabla ya mashindano kuanza.

 

Di Maria Akanusha Habari za Uongo.

Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid,  na Manchester United alishiriki chapisho la Instagram akidai kwamba yeye na mchezaji mwenzake wanataka kuepuka majeraha kabla ya Qatar 2022, hivyo watawaomba Juventus wasicheze dhidi ya Lazio mnamo Novemba 13.

Di Maria aliandika kwa kusema ni ‘Habari za uongo’, akiongeza emoji inayoeleza wazi kusikitishwa kwake  na habari hiyo . Mchezaji huyo alijiunga na Juventus msimu wa joto, na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na anaweza kurejea Rosario Central mnamo 2023.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa