Hans Flick ameionya timu yake ya Ujerumani kwamba makosa ya kibinafsi yatawagharimu kuelekea kwenye Kombe la Dunia baada ya matokeo yasiyoridhisha kwenye mechi mfululizo ya Ligi ya Mataifa dhidi ya Uingereza kwenye Uwanja wa Wembley.

 

Flick: Makosa ya mchezaji Binafsi Kutugharimu Kuelekea Kombe la Dunia

Ujerumani walikuwa wageni wa mchezo huo ambapo walianza kuongoza  kwa mabao mawili baada ya mkwaju wa penalti wa Ilkay Gundogan na bao la pili kutoka kwa  Kai Havertz katika kipindi cha pili.

Hata hivyo, vijana wa Hans Flick hawakukaa muda mrefu baada ya Uingereza kupata  mabao matatu ndani ya dakika 12 kutoka kwa Luke Shaw, Mason Mount na Harry Kane ambapo timu hiyo ya Southgate ikiwa imeshashuka daraja.

Makosa kutoka kwa mlinda mlango Nick Pope wa Newcastle United  yaliruhusu Havertz kufanya matokeo kuwa 3-3 baadaye, lakini kocha mkuu Flick alikiri Ujerumani lazima iwe bora kulinda bao la kuongoza nchini Qatar; Alisema kuwa,

 

Flick: Makosa ya Mchezaji Binafsi Kutugharimu Kuelekea Kombe la Dunia

“Matokeo haya yanasikitisha sana. Nadhani tulikuwa na utulivu sana baada ya 2-0 na tulifanya makosa ya kibinafsi, na unapaswa kusema kwamba England ilileta wachezaji wawili wapya ambao pia walishiriki katika kuifanya England kuwa na ufanisi zaidi kwa ushambuliaji,”

Flick alisema kuwa walifanya makosa ya kibinafsi na ndio maana inakatisha tamaa. Lazima tuangalie mchezo mzima na nadhani tulifanya mambo mengi vizuri, vizuri sana. Katika awamu ambayo tulipata mabao matatu, hilo halipaswi kutokea kwetu, kwa sababu hasa kwenye Kombe la Dunia, mambo kama hayo,  kwa kweli ni mabaya na unaondolewa haraka kuliko vile unavyofikiria

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa