Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique amesema mchezo wao wa leo dhidi ya Ureno ambao ndio utaamua nani aende nusu fainali ya Michuano ya Uefa Nations League wataucheza kama robo fainali ya kombe la dunia.

Hispania watacheza na mabingwa wa mataifa ya ulaya mwaka 2016 katika mchezo wa kundi A2 katika mchezo utakaopigwa jijini Braga nchini Ureno katika mchezo huu ambao utaamua nan aongoze kundi hilo ambalo mpaka sasa Ureno wakiwa kileleni na alama zao 10 huku Hispania wakiwa na alama zao 8.

luis Enrique
Luis Enrique – Hispania

Mchezo huu utaamua ni nani ataungana na kati ya Croatia, Uholanzi, pamoja na Italia katika nusu fainali ya michuano hiyo mechi ambayo Enrique anaiona kama Robo fainali ya kombe la dunia kutokana na ugumu wake.

Hispania walipoteza matuamaini nafasi ya kuongoza kundi hilo baada ya kufungwa katika mchezo uliopita baina yao na Uswisi kwa mabao mawili kwa moja wakiwa nyumbani.

“Ni fainali tunaifikiria hivo. Ni vema kufika mechi ya mwisho kukiwa na nafasi ya kua mabingwa”alisema Enrique jumatatu katika mahojiano na wandishi wa habari kabla ya mchezo.” – Luis Enrique

luis enrique“Tunaiweka kama robo fainali pale Qatar ni dakika 90 ambazo tunahitajika kushinda tu maana hata tukisuluhu haina manufaa kwetu“. – Luis Enrique

 

“Siku zote nawaona Ureno kama timu yenye vipaji na wenye utimamu wa kimwili. “Tayari wameshinda vitu muhimu sana na mabadiliko ya timu yanapimwa kutokana na vitu wanavyoshinda”. – Luis Enrique

Mchezo huo utapigwa usiku wa leo Ureno wakiwa nyumbani katika dimba la Estadio de Municipal Braga timu hizo  hua zikikutana mchezo hua unakua mgumu sana kati yao na ndio jambo ambalo linatarajiwa na wengi usiku wa leo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa