Mchezaji namba moja wa Tenisi Uingereza, Emma Raducanu alilazimika kutoendelea na mechi yake ya raundi ya kwanza ya Italian Open na Bianca Andreescu kutokana na jeraha la mgongo.

Mshindi huyo wa US Open 2021 na namba 12 kwa ubora duniani alikuwa nyuma kwa seti 6-2 2-1 wakati wa kujiondoa dhidi ya Mkanada huyo.

 

raducanu, Emma Raducanu Ajiondoa Italian Open., Meridianbet

Raducanu alijitahidi kumaliza seti ya kwanza, lakini mwanzoni mwa seti ya pili alionekana kukosa raha na wakati huu alichukua uamuzi wa kutoendelea akimwambia fizio wake “Siwezi kusogea.”

Raducanu, 19 amekuwa na matokeo mchanganyiko baada ya kushinda taji lake la kwanza la Grand Slam kwenye michuano ya US Open mwaka jana, Akifanikiwa kutinga robo fainali mjini Stuttgart na 16 bora Madrid Open.

Emma kwa sasa hana kocha wa kudumu baada ya kutengana na Torben Beltz mwezi uliopita, atakuwa na matumaini ya kurejea katika hali yake ya utimamu kamili wa mwili wakati michuano ya French Open itakapoanza huko Roland Garros chini ya wiki mbili zijazo.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa