Bingwa wa dunia wa Formula 1, Max Verstappen amekubali mkataba mpya wa muda mrefu na timu ya Red Bull huku mkataba huo ukitarajiwa kusainiwa mwishoni mwa wiki hii.
Mkataba huo wa pauni milioni 40 unatarajiwa kudumu kwa miaka sita mpaka mchezaji huyo atakapotimiza miaka 30 na kumfanya kulipwa sawa na mchezaji wa timu ya Mercedes, Lewis Hamiliton.
Verstappen alishinda taji lake la kwanza la ubingwa wa dunia mnamo 2021 baada ya kumshinda bingwa mara saba, Hamilton baada ya kumaliza kwa kutatanisha kwenye mashindano ya Grand Prix ya mwisho ya msimu ya Abu Dhabi mnamo Desemba.
Mholanzi huyo, ambaye mkataba wake wa sasa na Red Bull unamalizika 2023, ataanza kutetea taji lake Machi 20 msimu wa 2022 utakapoanza nchini Bahrain.
Mkataba mpya wa Verstappen utazuia Mercedes kutomnyatia kama mbadala wa Lewis Hamilton iwapo Muingereza huyo atastaafu mwishoni mwa mkataba wake wa sasa mwaka 2023.
Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.