Hakimi Yuko Sana PSG

Beki wa kulia wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Morocco Achraf Hakimi inaelezwa bado yupo sana ndani ya klabu hiyo ya mabingwa wa Ufaransa licha kutakiwa na vilabu kadhaa.

Beki Hakimi amekua akifukuziwa na vilabu kadhaa nje ya Ufaransa ambavyo ni klabu ya Man City pamoja na Man United,Lakini inaelezwa beki huyo hana mpango wa kuondoka klabuni hapo ndani ya dirisha hili la majira ya joto.HakimiWakala wa mchezaji huyo amezungumza na chombo kimoja nchini Ufaransa na kusema beki huyo akili yake kwasasa asilimia 100 ipo ndani ya PSG na hafikirii kuondoka ndani ya klabu hiyo ndani ya msimu huu.

Beki mwenyewe Achraf Hakimi amesema kua mkurugenzi wa klabu ya PSG bwana Ocampos  anajua kuhusu mustakabali wake na anaamini ataweka mambo sawa na hapo baadae ndipo atajua maisha yake ndani ya timu hiyo yatakuaje.HakimiAchraf Hakimi amekua kwenye ubora mkubwa kwa misimu miwili ambayo akitokea klabu ya Inter Milan ya nchini Italia, Kutokana na ubora huo ndio umesababisha mchezaji huyo kuanza kufuatliwa na vilabu mbalimbali kuhitaji huduma yake.

 

Acha ujumbe