Mbappe Arejeshwa Kikosi cha kwanza

Mshambuliaji wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe sasa ni rasmi amerejeshwa kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kuelekea michezo mingine.

Mbappe ikumbukwe aliondolewa kwenye kikosi cha klabu hiyo ambacho kilisafiri kuelekea Japan kwajili ya kujiandaa na msimu mpya, Lakini mapema leo taarifa inaeleza mchezaji huyo amerudishwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.MbappeTaarifa kutoka kutoka klabu ya PSG inaeleza kua kumekua na mazungumzo chanya baina ya mchezaji huyo na klabu yake hiyo kabla ya mchezo dhidi ya klabu ya Lorient uliopigwa jana na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mshambuliaji huyo alionekana kwenye vyumba vya kubadilishia nguo jana akiwa na wachezaji wenzake, Lakini pia mchezaji huyo ameonekana katika kiwanja cha mazoezi leo baada ya mchezo wa jana usiku dhidi ya Lorient ambapo hakua sehemu ya kikosi.MbappeMchezaji Kylian Mbappe amekua kwenye hali ya sintofahamu ndani ya kikosi cha PSG kwani mchezaji huyo aligoma kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo, Huku ikielezwa anataka kwenda klabu ya Real Madrid ambapo mpaka sasa inaelezwa anaweza akakubali kusalia ndani ya PSG baada ya mazungumzo kabla ya mchezo wa jana.

Acha ujumbe