Staa wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe ameonywa na gwiji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Guti kua atakapojiunga na klabu ya Real Madrid anapaswa kua mtulivu na kuweka kichwa chini.

Staa Kylian Mbappe ambaye amekua akihusishwa na kujiunga na klabu ya Real Madrid kwa kipindi kirefu amepta onyo kutoka kwa gwiji Guti kua endapo akijiunga na mabingwa hao watetezi wa ulaya, Kwani mchezaji huyo anaelezwa kupenda ukubwa anapokua kwenye timu.MbappeGwiji Guti amesema kua staa huyo akienda ndani ya Real Madrid anapaswa kua mtulivu na aweke kichwa chake chini kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, Kwani kuna wachezaji wengi wakubwa wamepita ndani ya klabu hiyo akiwataja wachezaji kama Luis Figo, pamoja Ronaldo ambao anaeleza walikua watulivu.

Gwiji Guti amesema kua hajui kinachoendelea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ndani ya klabu yake ya sasa ya PSG, Lakini Guti amemsisitiza mchezaji huyo kama ikitokea anajiunga ndani ya Real Madrid basi awe mtulivu na aweke kichwa chini kwani Real Madrid ni kubwa kuliko mchezaji.Mbappekylian Mbappe bado anaelezwa kua ana uwezekano mkubwa wa kujiunga na klabu ya Real Madrid licha ya kusaini mkataba mpya na klabu ya PSG mwishoni mwa msimu uliomalizika, Lakini inaelezwa nyota huyo bado na yeye ana ndoto za kujiunga na Real Madrid kwani ni klabu ya ndoto zake.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa