Winga wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga klabu ya PSG ya nchini humo Kylian Mbappe imearifiwa kua yuko mbioni kuuzwa katika dirisha hili la majira ya joto.
Mbappe ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili ndani ya klabu hiyo dirisha kubwa lililomalizika na kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja, Winga huyo mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu ujao.
Winga huyo alisaini mkataba wa miaka miwili ndani ya klabu hiyo msimu ulimalizika ambao utamueka klabuni hapo mpaka mwaka 2024 na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja mpaka mwaka 2025, Lakini mchezaji huyo ameiandikia klabu hiyo barua na kuwaeleza kua kile kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja mpaka 2025 hatausaini.
Kylian Mbappe baada ya kuwaeleza klabu ya PSG kua hataongeza mkataba wa kuendelea kusalia klabunu hapo, Klabu hiyo imeanza kufikiria kumuuza mchezaji huyo kwani haipo tayari kumuona mchezaji huyo anaondoka bure mwisho wa msimu ujao Juni 2024.
Klabu ya PSG ipo tayari kumuuza Mbappe katika dirisha hili kwani imeshatambua fika mchezaji huyo hataongeza mkataba na wakimuacha basi ataondoka bure mwishoni mwa msimu ujao, Huku taarifa zikieleza kua mchezaji huyo anataka kujiunga na klabu ya Real Madrid.

