Gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Everton na timu ya taifa ya Uingereza Phil Neville amesema nyota wa klabu ya PSG Lionel Messi akijiunga na ligi kuu ya Marekani utakua usajili wa kihistoria.
Phil Neville ambaye kwasasa ni kocha wa klabu ya Inter Miami inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani maarufu kama MLS anaamini ujio wa Lionel Messi kwenye ligi kuu ya Marekani utakua na mvuto wa ajabu na utaweka historia kubwa.
Lionel Messi ambaye anakipiga ndani ya miamba ya soka nchini Ufaransa kwasasa anawindwa na klabu ya Inter Miami kwa kiasi kikubwa, Inaelezwa klabu hiyo inamuwinda staa huyo tangu dirisha lililopita na bado wako tayari kumshawishi dirisha kubwa linalofata.
Kocha Phil Neville anaona pia sio mbaya kwa mchezaji huyo kujiunga na ligi kuu Marekani kwani atakua anafuata nyayo za wachezaji wenzake wakubwa mbalimbali ambao wamewahi kupita ligi kuu ya Marekani kama Andrea Pirlo, Steven Gerrard, David Beckham, na Zlatan Ibrahimovic.
Klabu ya PSG ipo mezani na nyota Lionel Messi kwajili ya kumuongezea mkataba mpya staa huyo hivo klabu ya Inter Miami itakutana na ushindani mkali kutoka kwa wababe wa ligi kuu ya Ufaransa, Lakini mwisho wa siku mchezaji huyo ndio ataamua hatma yake kusalia PSG au kutimkia MLS.

