Aliyekuwa kocha wa zamani wa PSG, Mauricio Pochettino amesema kwamba Kylian Mbappe analazimikakuondoka kwenye timu yake ya sasa ili kujiendeleza kwenye kugombea Ballon d’Or Duniani.

Mshindi wa Kombe la Dunia Mbappe 2018, ambaye atajaribu kusaidia Ufaransa kutetea taji lao nchini Qatar, mara kwa mara amekuwa akihusishwa na kuondoka Parc des Princes kwenda Real Madrid.

Mabingwa hao wa Uhispania na Ulaya walionekana kutaka kumnasa Mbappe kwenda Madrid kwa uhamisho wa bila malipo kabla ya msimu wa 2022-23, lakini mshambuliaji huyo akasaini mkataba mzuri zaidi wa miaka mitatu na PSG mwezi Mei.pochettinoKutokuwa na uhakika zaidi kulificha mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 huku ripoti mpya za kutoridhika zilipoibuka mwezi Oktoba, ingawa Mbappe alihakikisha kwamba ahadi yake itasalia katika mji mkuu wa Ufaransa.

Hata hivyo, Mauricio Pochettino alipendekeza mshambuliaji huyo wa zamani wa Monaco atalazimika kusonga mbele ili kutambua uwezo wake wa kiwango cha Kimataifa.

Pochettino aliliambia gazeti la Uhispania El Pais: “Anaweza kuwa kiongozi kwa sababu kila mtu anamuona kuwa mshambuliaji bora zaidi duniani, lakini leo hii tuzo ya Ballon d’Or imechukuliwa na Benzema, ambaye ni Mfaransa kama yeye. Mageuzi ya Mbappe yanatokana na kuondoka klabuni hapo.”

Pochettino aliongeza kwa kusema kuwa upya wa PSG ni jambo zuri kwa klabu na mshabiki wake, lakini Mbappe katika siku zijazo atalazimika kuzingatia kwamba kuacha starehe kutamleta karibu na kupigania Ballon d’Or.pochettinoMbappe amezifumania nyavu mara 19 katika mechi 20 alizochezea PSG msimu huu, idadi hiyo ikifanywa na Erling Haaland (23) wa Manchester City pekee miongoni mwa wachezaji katika ligi tano bora za Ulaya.

Nyota huyo wa PSG alikua chipukizi wa pili kufunga bao kwenye fainali ya Kombe la Dunia (baada ya Pele mwaka 1958) katika michuano yake mikubwa ya Kimataifa mwaka wa 2018, ingawa Pochettino anaamini Mbappe bado “hajakomaa”.

Mbappe ni mdogo kuliko Messi na Neymar na bado hajakomaa lakini ameshinda Kombe la Dunia na ana haiba kubwa lakini bado anahitaji kujitafuta. Lionel Messi na Neymar ni wachezaji kamili, wanawajibika zaidi ingawa kwa njia tofauti.

Mbappe na wachezaji wenzake wataanza kampeni yao ya Kombe la Dunia huku dhidi ya Australia katika mpambano wa Kundi D Jumanne.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa