Kocha wa zamani wa klabu ya PSG na Tottenham ya nchini Uingereza Mauricio Pochettino amefunguka kua suala la yeye kupata kibarua kipya ni kuvuta subira kwani anaamini kila kitu kina muda wake.

Kocha huyo ambaye alitumuliwa katika klabvu ya Chelsea mwishoni mwa msimu uliomalizika baada ya kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo kwenye ligi ya mabingwa ulaya msimu uliomalizika na kutolewa na Real Madrid kwene hatua ya 16 bora.pochettinoKocha huyo amekua akihusishwa na vilabu vya Real Madrid na Manchester United ambapo klabu ya Real endapo Anchelotti ataondoka na huku kwa Man United ambayo wao walimchagua kocha wa sasa Eric Ten Haag.

Pochettino alipoulizwa mipango yake ipoje juu ya vilabu hivo yeye alijibu kua kila kitu ni suala la muda huku akiamini ikifika muda sahihi basi atapata nafasi kwenye klabu ambayo anaamini ni bora na yenye hadhi yake.pochettinoKocha Pochettino pia amekua akihusishwa na kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Uingereza endapo kocha wasasa Gareth Southgate atamaliza muda wake lakini ameendelea kusisitiza kwenye muda muafaka ukifika basi atarudi kufanya kazi kama kawaida.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa