Golikipa wa Arsenal Aaron Ramsdale amesema kuwa Bukayo Saka anaweza kustawi wakati wa kampeni ya Kombe la Dunia la Uingereza baada ya kukabiliana na tatizo la kukosa penalti kwenye fainali ya Euro 2020.

 

Ramsdale: Saka Anaweza Kufanikiwa Kombe la Dunia

Mkwaju wa penalti wa Saka uliokolewa na Gianluigi Donnarumma baada ya sare ya suluhu ya England na Italia Julai iliyopita, na hivyo kuhakikisha Three Lions walipoteza mechi yao ya kwanza kuu ya fainali tangu Kombe la Dunia la 1966.

Winga huyo baadaye alivumilia masikitiko zaidi kwenye hatua ya ndani huku Arsenal ikishindwa kumaliza katika nafasi ya nne bora muhula uliopita, lakini amerejea kwenye kiwango kizuri msimu huu.

Alipoulizwa na ESPN kuhusu Saka Ramsdale alisema kuwa;“Ni kijana mzuri, anafanya kazi kwa kila wiki, na mara chache sana hukosa mafunzo na alitumia motisha ya ukosoaji wote lakini pia upendo ambao kila mtu alimpa ulimtia nguvu.”

Ramsdale: Saka Anaweza Kufanikiwa Kombe la Dunia

Aliongezea kwa kusema kuwa alikuwa na shinikizo la klabu nzima ya soka mwaka jana yeye na Emile Smith Rowe na amekabiliwa na hilo, ameshughulikia kila kitu kingoine.

Mchezaji huyo pia alijilaumu kwa timu yake kushindwa kufuzu kwa Ligi ya mabingwa barani Ulaya . Huku Arsenal walipokosa nafasi ya nne bora, alihisi kama makosa yake yote

Aliendelea kusema msimu uliopita walimaliza nafasi ya tano, na kama wakipiga hatua nyingine tena, watakuwa katika nafasi nne za juu japokuwa ni mchezo wa soka kuna mengi zaidi ya hilo.

Ramsdale: Saka Anaweza Kufanikiwa Kombe la Dunia

Alipoulizwa kama Saka amekuwa mhusika mwenye nguvu zaidi katika mwaka uliopita, aliongeza: “Hakika hakuna shaka kuhusu hilo, nje ya uwanja na juu yake, yeye ni mtu kamili zaidi.”

Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Ramsdale, Ramsdale: Saka Anaweza Kufanikiwa Kombe la Dunia, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa