Arsenal wameendelea kuwa na matokeo mazuri kwenye michezo 9 mfululizo. Mafanikio ya The Gunners, ni matokeo ya Aaron Ramsdale kuibeba timu mabegani mwake.
Kwa sehemu kubwa, matokeo ya Arsenal yanachagizwa na ubora wa Ramsdale katika kulinda lango lake. Hii imejidhihirisha zaidi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Leicester City.
Arsenal wameibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 2-0, magoli ambayo yamefungwa kwenye kipindi cha kwanza.

Licha ya The Gunners kushinda, Aaron alikua shujaa wa Mikel Arteta. Akiwa golini kama mlinzi wa 5 baada ya walinzi wanne mbele yake, Aaron ameokoa jumla ya nafasi 8 za magoli ambayo Leicester City walizipata kwenye mchezo huo.
Kujisahau kwa Leicester, kulikuwa faida ya Arsenal kwenye kipindi cha kwanza. Wakati The Foxes wanarejea mchezoni, walikutana na uhodari wa Aaron golini.
JIUNGE KWENYE SHINDANO LETU LA EXPANSE NA USHINDE!
Achana na ndoto za usingizini za kuokota burungutu la pesa, amkia upande wa ushindi halisi kutoka Meridanbet kwenye shindano la Expanse linalojumuisha michezo pendwa ya sloti za mtandaoni iliyopo kwenye promosheni ya Expanse kutoka Meridianbet.


