Klabu ya soka ya Simba leo itashuka dimbani kumenyana na Maafande kutoka Mlandizi klabu ya Ruvu Shooting mchezo utakaopigwa kwenye uwanja Benjamin Mkapa huku Ruvu wakiwa wenyeji wa mchezo huo.

Klabu ya Ruvu Shooting ambao ndo wenyeji wa mchezo huo leo wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu za kupoteza michezo yote miwili ya ligi kuu dhiidi ya mnyama msimu uliomalizika. Kupitia msemaji wa klabu hiyo Masau Bwire anaamini wana timu nzuri ya kwenda kuchukua alama tatu mbele ya Mnyama.simbaKlabu ya Ruvu watahitaji sana alama tatu za mchezo wa leo kwani wametoka kupoteza mchezo uliomalizika dhidi ya Azam katika dimba la Chamazi Complex kwa bao moja kwa bila lililofungwa na mshambuliaji Idris Mbombo kwa mkwaju wa Penati.

Klabu ya Simba wao wanaelekea kwenye mchezo huu wakitaka kuendelea walipoishia kwenye michezo miwili iliyopita wakifanikiwa kupata matokeo mazuri katikia dimba la Benjamin Mkapa.simbaPia Simba wanakwenda kwenye mchezo huo dhidi ya Ruvu Shooting huku rekodi zikiwabeba kwani kwenye michezo 10 ya mwisho vilabu hivo kukutana mnyama amefanikiwa kushinda mara nane huku akipoteza mara moja na kusare mchezo mmoja. Hivo wekundu wa msimbazi rekodi zinawabeba kuelekea mchezo huo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa