Mchezaji wa Brazil Vinicius Junior alihofia kwamba angekosa kampeni ya Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya Taifa kutokana na majeraha baada ya kulengwa na changamoto “chafu” katika maandalizi ya michuano hiyo.

 

Vinicius Alihofia Kukosa Kombe la Dunia Kutokana na Majeraha

Winga huyo wa Real Madrid amechangia mabao tisa katika LaLiga msimu huu (mabao sita, asisti tatu), ambapo  idadi hiyo ikifungwa na Robert Lewandowski (17) na Borja Iglesias (10).

Vinicius pia ameshinda mechi 16 za wakubwa akiwa na Brazil baada ya kucheza mechi yake ya kwanza ya Kimataifa mnamo 2019, akiibuka kama sehemu muhimu ya timu ya Tite kabla ya mashindano nchini Qatar.

Huku upangaji wa ratiba ya Kombe la Dunia katikati ya msimu ukishutumiwa baada ya wachezaji kadhaa wenye majina makubwa akiwemo Sadio Mane na Paul Pogba kuondolewa kutokana na jeraha, Vinicius anasema yeye na mchezaji mwenzake Rodrygo walilengwa kwa changamoto zisizofaa na wapinzani.

Vinicius Alihofia Kukosa Kombe la Dunia Kutokana na Majeraha

Vinicius aliiambia Reuters; “Kinachotokea uwanjani husalia uwanjani, lakini kilienda mbali sana, unaweza kuja kwa nguvu, lakini walikuwa wachafu na changamoto zao. Rodrygo na mimi tuliteseka sana katika mechi hizo za mwisho na tuliogopa mbaya zaidi, kupata majeraha na kukosa Kombe la Dunia.”

Winga huyo aliendelea kusema kuwa unapoanza kuwa mchezaji muuhimu, wapinzani wanakufuata kwa bididd zaidi na lazima ujifunze kukabilian na hilo. Alijifunza mengi kutoka kwa Neymar alipokuwa akiichezea Barcelona kwani aliteseka sana pia Ronaldo alipokuwa Real aliteseka.

Karim ndiye alimwambia Vinicius awe na amani ya moyo kwasababu wapinzani wakikufukuza ni kwasababu unahusika na kwasababu wanakuogopa kwahiyo ndiyo maana anapochukua mpira na kwenda mbele hulipiza kisasi, na anasema kuwa amejiandaa kwa changamoto.

Vinicius Alihofia Kukosa Kombe la Dunia Kutokana na Majeraha

Brazil wanaanza harakati zao za kuwania Kombe la Dunia la sita watakapomenyana na Serbia siku ya Alhamisi, wakitarajia kulinda rekodi nzuri ya hatua ya makundi katika siku za hivi karibuni za michuano hiyo.

Selecao hawajafungwa katika mechi 15 zilizopita za makundi ya Kombe la Dunia, wakishinda 12 (D3), huku kichapo chao cha mwisho kama hicho kikitoka dhidi ya Norway mnamo 1998.

Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Vinicius, Vinicius Alihofia Kukosa Kombe la Dunia Kutokana na Majeraha, Meridianbet

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa