Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez anaamini kupoteza dhidi ya timu ya taifa ya Misri siku ya jana inaweza kua kipimo kizuri kuelekea michuano ya kombe la dunia nchini Qatar ndani ya wiki hii.

Timu ya taifa ya Ubelgiji jana ilipokea kipigo cha mabao mawili kwa moja katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na kombe la dunia, Magoli ya Mohamed Trezeguet na Mostafa Mohamed yalitosha kuizamisha Ubelgiji katika mchezo huo.martinezKocha Martinez anaamini kipigo hicho kitawashtua kutoka usingizini kwani wachezaji hawakuonesha kama wako tayari kuelekea michuano ya kombe la dunia, Hivo baada ya kupoteza mchezo huo itawarudisha na kuwakumbusha wanaelekea kwenye michuano mikubwa na kuonesha utayari.

Timu ya Ubelgiji ni timu namba mbili kwa ubora kwenye viwango vya ubora wa shirikisho la soka duniani FIFA hivo iliwashtua watu kidogo baada ya kupoteza mchezo dhidi ya timu ambayo haikufuzu michuano ya kombe dunia mwaka huu.martinezKocha Martinez pamoja na mchezaji wake Dries Mertens anayekipiga katika klabu ya Napoli wanaamini kupoteza mchezo sio vizuri lakini bora imetokea mapema kuliko ingetokea kwenye michuano ya kombe la dunia, Kupitia kauli hiyo inaonesha Misri imekua kipimo sahihi kwa Ubelgiji kuelekea Qatar.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa