Klabu ya PSG mabingwa watetezi wa wa ligi kuu ya Ufaransa wameweka wazi hawana mpango na kiungo wa kimataifa wa Morocco Azzedine Ounahi anayekipiga Angers.

Klabu ya PSG chini ya mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Ocampos wameweka wazi hawana mpango wa kumsajili kiungo anayekipiga katka klabu ya Angers inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa pia. Zaidi wanawekeza kwenye vijana walioko ndani ya klabu hiyo.PSGKiungo Azzedine Ounahi ambaye amefanya vizuri zaidi kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka jana nchini Qatar amekua akivitoa udenda vilabu mbalimbali barani ulaya na mabingwa hao wa Ufaransa wakihusishwa, Lakini klabu hiyo imeweka wazi kwenye mradi wao mchezaji huyo hana nafasi.

Kiungo Azzedine Ounahi ameingia kwenye rada ya vilabu mbalimbali kutokana na uwezo ambao aliionesha kwenye michuano ya kombe la dunia. Huku akifanikiwa kuiwezesha timu yake ya taifa ya Morocco kua timu ya kwanza ya Afrika kufika nusu fainali ya michuano hiyo.PSGKlabu ya PSG imekanusha kumuhitaji kiungo huyo anayekipiga Angers ya nchini Ufaransa, Huku klabu hiyo ikisisitiza kua inaandaa vipaji vyao na wanamuandaa kijana Zaire Emery kwenye nafasi kwa matumizi ya baadae kwenye klabu hiyo badala ya Azzedine Ounahi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa