Guiffredi Amuwashia Moto Vikali Antonio Conte

Wakala wa wachezaji, Mario Guiffredi, amemshambulia vikali kocha Antonio Conte akimtuhumu kukosa ujasiri wa kutumia vipaji vijana na kuwafanya kuwa kama mateka ndani ya kikosi. Kauli hiyo kali imekuja baada ya Napoli kupata matokeo mengine yasiyoridhisha ya 1–1 ugenini dhidi ya Copenhagen.

Mario Guiffredi alitoa kauli hizo katika mahojiano na Calcio Napoli 24, akieleza wazi kutoridhishwa kwake na namna Conte anavyosimamia kikosi, hususan matumizi ya wachezaji vijana. Guiffredi anawakilisha wachezaji kadhaa wa Napoli akiwemo nahodha Giovanni Di Lorenzo, Matteo Politano, Antonio Vergara pamoja na vijana Marianucci na Ambrosino, hali inayofanya kauli zake zizidi kuwa na uzito ndani ya kambi ya Il Partenopei.

Guiffredi Amuwashia Moto Vikali Antonio Conte

Napoli imekuwa ikikumbwa na majeruhi ya wachezaji wakubwa msimu huu, hali iliyodhoofisha kampeni yao ya Ulaya na harakati za kutetea taji la Serie A. Majina makubwa kama Romelu Lukaku, Kevin De Bruyne, Zambo Anguissa, Alex Meret na Billy Gilmour yamekosa michezo mingi, huku Politano naye akiwa nje kwa muda. Kwa sasa Napoli ipo nafasi ya 23 kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa, ikielekea kwenye raundi ya mchujo, na pia ipo pointi sita nyuma ya Inter kileleni mwa Serie A.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Licha ya changamoto hizo, Guiffredi anaamini Conte ameshindwa kutumia kikosi chake ipasavyo. Ni Antonio Vergara pekee aliyepewa nafasi ya mara kwa mara, akianza michezo miwili ya mwisho ikiwemo sare dhidi ya Copenhagen. Kwa upande mwingine, Marianucci mwenye umri wa miaka 21 amecheza mechi mbili tu msimu huu, huku Ambrosino akionekana katika michezo mitano pekee.

Guiffredi Amuwashia Moto Vikali Antonio Conte

Akisisitiza hasira yake, Guiffredi alimtaka Conte ajifunze kutoka kwa makocha wengine wa Serie A wanaoamini vijana. Alisema: “Sitakubali kubezwa. Kama Conte hana ujasiri wa kutumia vijana, hilo si tatizo langu. Allegri anawapa nafasi vijana Milan, Atalanta na Inter wanafanya hivyo pia. Conte anatakiwa aamue kama Marianucci na Ambrosino ni wachezaji wa Napoli. Kama ndivyo, basi awe na ujasiri wa kuwapa nafasi halisi, si dakika chache mara chache. Vinginevyo, awaache waende kuthibitisha uwezo wao kwingineko.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.