Allegri: Namuonea Huruma Pogba

Kocha wa klabu ya Juventus Massimiliano Allegri amesema anamuonea huruma kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba kutokana na mashatka ambayo yanamkabili hivi sasa.

Kocha Allegri anasema kua wanahitaji kusubiri mpaka kwakua kuna uchunguzi unaendelea kutokana na sakata ambalo linamuandama kiungo Paul Pogba mpaka.allegriPaul Pogba ameandamwa na shutuma za kujihusisha na utumizi wa dawa za kuongeza nguvu mchezoni,Hivo hali imemfanya kiungo huyo kua na wakati mbaya sana mpaka wakati huu kwani shutuma hiyo ni nzito.

Kiungo Paul Pogba alibainika kua anatumia madawa ya kuongeza nguvu mchezoni katika mchezo dhidi ya Udinese tarehe 20 mwezi Agosti, Hivo mamlaka inayohusika na utumizi wa dawa za kuongeza nguvu mchezoni ikatoa taarifa kuthibitisha jambo hilo.allegriLicha ya taarifa kuthibitishwa na mamlaka husika nchini Italia juu ya kiungo Paul Pogba kuhusika na utumizi wa dawa za kuongeza nguvu mchezoni, Lakini kocha Allegri anasema kuna uchunguzi ambao unaendelea ili kuthibitisha zaidi kinachoendelea kwa Pogba.

 

Acha ujumbe