Nini Kimeikumba Juventus Mpaka Rais Wao Kujiuzulu?

Bodi nzima ya wakurugenzi wa Juventus wamejiuzulu nyadhifa zao kwa kushangaza, akiwemo rais Andrea Agnelli na makamu wa rais Pavel Nedved.

 

juventus

 

Uamuzi wa pamoja umetolewa na bodi ya wakurugenzi wa miamba hao wa Italia kujiuzulu kwa wingi, na kuwaacha katika hali ya mtafaruku mashabiki na wapenzi wa timu hiyo, wakati wa mapumziko ya katikati ya msimu wa Kombe la Dunia. Beti na kitochi mechi za kombe la dunia, Bonyeza hapa.

Mkurugenzi Mtendaji Maurizio Arrivabene anatazamiwa kusalia kusimamia majukumu yake ya kiutawala licha ya kujiuzulu, huku klabu hiyo ikitarajiwa kuingia katika kipindi kikubwa cha mpito.

Msimu wa 2021-22 ulishuhudia hasara ya kuvunja rekodi iliyochapishwa na klabu ya Turin, na hasara ya £220million (€254.3m) ikiwa imesajiliwa.

Uamuzi wa kuondoka kwa bodi ambayo ilikuwa habari ya ukurasa wa mbele nchini Italia na dunia kwa ujumla, ilitolewa kwa pendekezo la rais Agnelli, baada ya bodi kukubaliana kuwa ni kwa manufaa ya klabu kwa kundi jipya la watendaji, kuchukua mikoba ya Juventus.

Agnelli aliwaandikia barua wafanyakazi wote wa Juventus ambapo alitangaza ‘matokeo ya ajabu’ ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja wao wa Allianz, pamoja na mataji tisa mfululizo ya ligi kwa timu ya wanaume na matano mfululizo kwa upande wa wanawake.

 

juventus

Pia alizungumza kuhusu mechi za fainali za Ligi ya Mabingwa mjini Berlin na Cardiff na kisha akasema: “Tunakabiliwa na wakati mgumu katika jamii. Afadhali kuwaacha wote pamoja, kutoa uwezekano kwa timu mpya kupindua mchezo”.

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

Barua yake, iliyotumwa kwa wafanyikazi wote kabla ya kujiuzulu, iliendelea: “Wakati timu haijashikamana inajitolea kwa wapinzani na hii inaweza kuwa mbaya.

“Kwa wakati huo tunahitaji kuwa na uwazi na kudhibiti uharibifu. Nitaendelea kufikiria na kufanyia kazi klabu bora zaidi ya soka, nikifarijiwa na msemo wa Friedrich Nietzsche: “Na wale waliojiona wakicheza walichukuliwa kuwa wazimu na wale ambao hawakusikia muziki”.

“Kumbuka kila mtu, tutatambuana kila mahali kwa sura, sisi ni watu wa Juve!”

Maelezo ya barua hiyo yalitolewa na Ansa na La Repubblica.

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari vya Italia, uamuzi huo kwa kauli moja unakuja kutokana na kuhusika katika uchunguzi wa Prisma, uliofunguliwa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma wa Turin kwa matumizi mabaya ya fedha na udanganyifu wa masoko.


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

CHEZA HAPA

 

juventus

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.