Osimhen Hataki Kusalia Napoli

Mshambuliaji wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen inaripotiwa hataki kubaki ndani ya klabu hiyo mabingwa wa soka nchini Italia kwa muda mrefu zaidi.

Osimhen alikua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Napoli na kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo baada ya miaka mingi kupita amefanikiwa kubakia ndani ya klabu hiyo baada ya dirisha kufungwa, Lakini mpango wake sio kusalia zaidi ndani ya klabu hiyo.osimhenKlabu ya Napoli chini ya Rais Aurello de Laurentiis wako kwenye mkakati wa kumuongezea mkataba mpya na mshahara mchezaji huyo ili kumshawishi aendelee kusalia kwa muda mrefu ndani ya viunga vya Diego Armando Maradona.

Mshambuliaji huyo ambaye alikua gumzo kwenye dirisha la usajili lililopita alihitajika na vilabu mbalimbali inaelezwa amekubali kuongezewa mshahara mkataba ambao pia utamuongezea maslahi kwenye mshahara wake.osimhenNapoli wameamua kutaka kumuongezea mkataba mpya mchezaji mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu ili kuepuka usumbufu katika dirisha dogo la mwezi Januari, Taarifa zinaeleza mpaka sasa Osimhen amekubali vipengele vya mkataba mpya kasoro kipengele cha kiasi kitachomruhusu kumuachia ndani ya timu hiyo ndio muafaka haujafikiwa.

Acha ujumbe