Simba Yashutumiwa kudanganya na Ngome Fc

Klabu ya Simba imeshutumiwa na klabu ya Ngome ambayo wamecheza nao mchezo wa kirafiki leo kwajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika.

Klabu ya Ngome imeishtumu Simba kwa taarifa za uongo ambazo imetoa kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, Ambapo klabu hiyo imekanusha kufungwa mabao sita kwa bila na Wekundu wa Msimbazi kama walivyoeleza kwenye mitandao yao ya kijamii.simbaWekundu wa Msimbazi mapema leo walicheza mechi ya kirafiki katika uwanja wao wa Mo Arena unaopatikana Bunju jijini Dar-es-salaam na kueleza kua wamefanikiwa kushinda kwa mabao sita kwa bila dhidi ya Ngome jambo ambalo klabu hiyo wamekanusha kupitia taarifa kwa umma waliyoitoa.

Klabu ya Ngome Fc imesema Wekundu wa Msimbazi wana nia ya kushusha hadhi ya klabu hiyo kutokana na taarifa ambayo wameitoa, Hivo wakiitaka klabu hiyo kuhakikisha wanakanusha taarifa hiyo na kufuta taarifa hiyo kwenye mitandao yao ya kijamii ndani ya masaa 24.simbaKlabu ya Simba mpaka sasa haijatoa tamko lolote juu ya shutuma ambazo zimetolewa na klabu ya Ngome ili kuthibitisha kua tuhuma hizo ni za kweli au sio kweli kwani mpaka sasa Wekundu wa Msimbazi hawajatoa taarifa yeyote.

Acha ujumbe