Arsenal Bado Mazungumzo Yanaendelea na Odegaard

Arsenal bado wanaendelea kufanya mazungumzo na nahodha wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Norway Martin Odegaard kwajili ya kumpa mkataba wa muda mrefu wa kuendelea kusalia Emirates.

Klabu ya Arsenal inaendelea kuhakikisha inawabakiza nyota wake waliopo ndani ya klabu hiyo kwa misimu mingi zaidi kwakua wana malengo ya muda mrefu na wachezaji hao kupitia kwa kocha Mikel Arteta.arsenalKocha Mikel Arteta anaamini kiungo huyo wa kimataifa wa Norway ni moja wa wachezaji muhimu ambao anastahili kuendelea kua nao kwa misimu ya mbeleni ndani ya klabu hiyo na ndio sababu anahitaji mchezaji huyo asaini kandarasi mpya.

Kiungo huyo amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu hiyo kwa misimu mitatu sasa, Kama Odegaard atafanikiwa kusaini mkataba mpya na timu atakua mchezaji wa sita wa kikosi cha kwanza kusaini mkataba mpya baada ya Saliba, Gabriel, Martinelli, Saka na Ramsdale.arsenalArsenal mipango yao ni kuhakikisha wanaendelea kutoa ushindani mkubwa katika ligi kuu ya Uingereza pamoja na ulaya kwa ujumla, Hivo mpango ni kuweza kuendelea kuwamiliki wachezaji wake muhimu na ndio maana wanahakikisha wanawapa mikataba mpya.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.