Arsenal Yaibuka Kidedea Yaipasua United

Klabu ya Arsenal imefanikiwa kuibuka kidedea katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuichapa Man United kwa jumla ya mabao matatu kwa moja katika mchezo uliopigwa katika dimba la Emirates.

Mabao ya Martin Odegaard, Declan Rice na Gabriel Jesus yalifanikiwa kuwapa Arsenal alama tatu muhimu katika dimba la nyumbani, Huku bao pekee la Manchester United likiwekwa kimiani na Marcus Rashford.arsenalManchester United ndio waliofanikiwa kupata bao mapema kupitia kwa Marcus Rashford kabla ya vijana wa Mikel Arteta kurejea na kusawazisha bao kupitia kwa nahodha wa klabu hiyo Martin Odegaard.

Mchezo huo ambao ulikua na matukio kadhaa ya utata ambapo Washika mitutu walipata penati kupitia kwa Kai Havertz ambayo ilikuja kukataliwa kupitia usaidizi wa VAR, vilevile Manchester United nayo walifunga bao kupitia kwa Alejandro Garnacho ambalo pia lilikataliwa.arsenalKlabu ya Arsenal wanaendelea kubaki kwenye orodha ya timu ambazo hazijapoteza mchezo mpaka sasa ambapo wamecheza michezo minne na kushinda mitatu huku wakisuluhu mmoja wakifanikiwa kujikusanyia alama 10 mpaka sasa.

Acha ujumbe