Klabu ya Arsenal wakiwa katika dimba lao la nyumbani la Emirates watawakaribisha vijana wa Erik Ten Hag katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza mkondo wa nne.
Arsenal wakiwa hawajapoteza mchezo mpaka sasa katika ligi kuu ya Uingereza watamenyana na Manchester United ambayo tayari imeshaonja uchungu wa kupoteza mchezo msimu katika mchezo, Mchezo huu unatarajiwa kua mkali kwakua vilabu vyote vitajitaji kupata matokeo ya ushindi.Mchezo wa mwisho uliovikutanisha vilabu hivyo Washika mitutu wa London walifanikiwa kupata matokeo ya ushindi na walikua kwenye uwanja waao wa nyumbani kama ilivyo kinachosubiriwa ni kama wataendelea walipoishia au Man United watabadilisha matokeo.
Klabu ya Manchester United wao walipokutana na Arsenal msimu uliomalizika klabu hiyo haikua imepoteza mchezo kama ilivyo msimu huu na wao ndio wakawavunjia rekodi hivo inasubiriwa pia kama Man United watavunja rekodi tena leo au watashindwa.Mchezo ambao unakutanisha vilabu hivi mara nyingi hua mchezo mkali na wakukata na shoka kwani vilabu hivi ni moja ya vilabu venye historia kubwa kwenye ligi kuu ya Uingereza lakini pia wana upinzani mkali baina yao.