Mason Greenwood Akumbana na Vikwazo Hispania

Winga wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood ambaye amesajiliwa kwa mkopo na klabu ya Getafe ya nchini Hispania amekumbana na vikwazo tena nchini Hispania.

Mason Greenwood amekumbana na vikwazo kutoka kwenye shirika linalopinga unyanyasaji nchini Hispania linalofahamika kama Anna Bella limeitaka klabu ya Getafe kutengua uamuzi wao wa kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza.mason greenwoodShirika hilo limeitaka Getafe kuachana na mchezaji huyo kwani kumsajili mchezaji huyo wao wanaona kama klabu hiyo imeunga mkono kitendo alichokifanya mchezaji huyo miaka miwili iliyopita.

Taarifa kutoka shirika hilo linaeleza uamuzi wa Getafe kumsajili mchezaji huyo ni kuonesha mfano mbaya kwa jamii, Kwani Getafe ni taasisi ambayo inaangaliwa na wengi hivo kumchukua mchezaji ambaye alikua na shutma za unyanyasaji wa kijinsia.mason greenwoodWinga Mason Greenwood alikua anakabiliwa na mashtaka ya kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia mpenzi wake, Lakini mahakama ilithibitisha kutupilia mbali madai hayo mwezi Febuari mwaka lakini ni jambo ambalo limekua likimsumbua mchezaji huyo kwasasa.

 

Acha ujumbe