Nahodha wa klabu ya Manchester United kiungo Bruno Fernandes raia wa kimataifa wa Ureno amechaguliwa mchezaji bora wa mwezi Agosti wa klabu hiyo kutokana na kiwango bora alichokionesha.

Bruno Fernandes amekua kwenye ubora mkubwa katika michezo mitatu Man United waliyocheza licha ya kupoteza mchezo mmoja,Lakini kiungo huyo ameonesha ubora mkubwa katika michezo mitatu aliyocheza.Bruno fernandesManchester United wamecheza michezo mitatu mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Uingereza wakifanikiwa kushinda miwili na kufungwa mchezo mmoja, Lakini katika michezo miwili waliyoshinda kiungo huyo ambaye ni nahodha wa klabu hiyo alikua kwenye ubora mkubwa.

Nahodha huyo amekua kwenye ubora mkubwa tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2020 mwezi Januari, Lakini siku za hivi karibuni kumekua na maneno kiungo huyo ameshuka kiwango lakini ameamua kujibu shutma hizo kwa vitendo.Bruno fernandesNahodha Bruno Fernandes ametangazwa kua mchezaji bora wa klabu hiyo kuelekea mchezo wao wa ligi kuu ya Uingereza jioni ya leo dhidi ya klabu ya Arsenal katika dimba la Emirates na kuangalia kama kiungo huyo ataendelea alipoishia.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa