Winga wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Mason Greenwood atarejea ndani ya klabu hiyo baada ya kutolewa kwa mkopo kwenda klabu ya Getafe.
Imefahamika kua Mason Greenwood ataitumikia klabu ya Getafe inayoshiriki ligi kuu ya Hispania kwa msimu huu mzima, Lakini baada ya hapo atarejea kunako klabu ya Manchester United.Winga huyo ambaye alikua nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia ambzo zilikua zinamkabili lakini zilipigwa chini na mahakama kwani alibainika hakua na hatia.
Hapo awali taarifa ya Manchester United ilieleza imeamua kuachana na mchezaji huyo, Lakini baada ya taarifa za yeye kujiunga na Getafe zimeshtua wengi kwani kila mmoja aliamini Man United wameachana na mchezaji huyo moja kwa moja.Manchester United inaelezwa italipa zaidi ya aslimia 50 ya mshahara wa Mason Greenwood kwa kipindi chote atakachokuepo ndani ya klabu ya Getafe, Hivo ni wazi kabisa mchezaji huyo anarejea ndani ya viunga vya Old Trafford msimu ujao.