Hojlund Kukipiga Leo Sancho Nje

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United Rasmus Hojlund ana nafasi kubwa ya kukipiga leo katika mchezo dhidi ya Arsenal hiyo ni baada ya kuanzia nje katika mchezo huo.

Wakati Rasmus Hojlund akiwa kwenye nafasi nzuri ya kukipiga katika mchezo wa leo winga wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Uingereza Jadon Sancho atakosekana katika mchezo huo ikiwa haijafahamika sababu zilizomfanya akosekane katika mchezo huo.HojlundMshambuliaji Anthony Martial leo ataanza katika mchezo dhidi ya Arsenal ambapo utakua mchezo wake wa pili kuanza msimu huu, Huku mshambuliaji Rasmus yeye akianzia nje na kukiwa na matumaini makubwa ya kuingia katika mchezo huo.

Mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Denmark hajafanikiwa kucheza mchezo wowote na klabu ya Manchester United tangu ajiunge na timu hiyo akitokea klabu ya Atalanta ya nchini Italia sababu ikielezwa ni majeruhi hivo akicheza leo utakua mchezo wake wa kwanza na timu hiyo.HojlundMshambuliaji Hojlund amekua akisubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa Manchester United wakihitaji kumuona akiitumikia klabu hiyo, Kwani wana matumaini makubwa na mchezaji huyo na klabu hiyo imekua ikihitaji mshambulliaji matata ambaye atakua na ubora mkubwa.

Acha ujumbe