Liverpool Yaipasua Aston Villa

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kupata alama tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga klabu ya Aston Villa kwa mabao matatu kwa bila.

Mabao ya Dominik Szoboszlai, goli la kuifunga la beki Matty Cash na Mohamed Salah yalifanikiwa kuipatia Liverpool ushindi wake wa tatu msimu baada ya kucheza michezo minne ya ligi kuu ya Uingereza.LiverpoolKlabu ya Aston Villa wamekubali kupokea kichapo chake cha pili msimu huu baada ya kupigwa katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Newcastle leo tena wamepokea kichapo dhidi ya Majogoo wa Anfield.

Vijana wa Jurgen Klopp leo waliendelea walipoishia wiki iliyomalizika kwani wikiendi iliyomalizika walifanikiwa kupata ushindi dhidi ya Newcastle baada ya kutoka nyuma kwa bao moja na kushinda tena wakiwa na kadi nyekundu.LiverpoolKlabu ya Liverpool inaendelea kubaki kwenye orodha ya timu ambazo hazijapoteza mchezo wowote mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Uingereza msimu huu, Huku wakifanikiwa kufikisha jumla ya alama 10 baada ya kushinda michezo mitatu na kusuluhu mmoja.

Acha ujumbe