Klopp Akanusha Salah Kutimkia Al Ittihad

Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amezungumzia sakata la mshambuliaji wake Mohamed Salah juu ya kutimka klabuni hapo na kujiunga na Al Ittihad ya nchini Saudia Arabia.

Klopp amesema taarifa za Salah kuondoka klabuni hapo sio za kweli na hizo zilikua taarifa za vyombo vya habari, Huku akisisitiza kua mchezaji huyo bado yupo klabuni hapo na jambo hilo lisingeweza kutokea.kloppMshambualiji Mohamed Salah alikua anahusishwa kuondoka ndani ya klabu ya Liverpool na kujiunga na Al Ittihad wiki moja iliyopita, Lakini dili hilo halijafanikiwa mpaka dirisha la usajili linafungwa siku ya tarehe moja.

Klabu ya Al Ittihad wamefanikiwa kusajili wachezaji kadhaa kutoka barani ulaya hivo taarifa za kumtaka Mohamed Salah wengi waliamini kua ni za kweli kwakua wameshaonesha wana uwezo wa kufanya hivo ambapo wamefanikiwa kusajili wachezaji kama Karim Benzema na Fabinho.kloppBaada ya kauli ya Klopp kua mchezaji huyo hakua na mpango wa kuondoka klabuni hapo inaonesha kua Salah bado yupo sana klabuni hapo na bado ana mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Acha ujumbe