Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United Rasmus Hojlund hatimae atakua kwenye kikosi cha klabu hiyo wikiendi ijayo dhidi ya klabu ya Nottingham Forest.
Manchester United ambayo imepoteza mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Tottenham Hotspurs, Lakini klabu ya Man United imekua na tatizo katika eneo la ushambuliaji na Hojlund anaonekana kama kuja kua mkombozi.Mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Denmark anatarajia kuanza kuitumikia klabu hiyo wikiendi hii, Jambo ambao linasubiriwa kwa hamu sana kwani klabu hiyo inaonekana kua na changamoto kwenye eneo la ushambuliaji.
Kitu kikubwa kinachosubiriwa kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Atalanta ya nchini Italia ni namna ambavyo ataweza kuibadilisha klabu hiyo haswa kwenye eneo la ushambuliaji ambalo limekua butu.Mshambuliaji Rasmus Hojlund ambaye alifanya vizuri ndani ya klabu ya Atalanta ya nchini Italia, Kinachosubiriwa zaidi ni kuona kama ataweza kukifanya kwa ufasaha mkubwa ambacho alikua akikifanya ndani ya klabu ya Atalanta akiwa Man United.