Hojlund Kutambulishwa Old Trafford Kesho

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester Rasmus Hojlund aliesajiliwa kutoka klabu ya Atalanta nchini Italia atatambulishwa kesho katika dimba la Old Trafford.

Manchester United kesho watakua na mchezo wa mwisho wa kirafiki kabla ya msimu kuanza ambapo watakipiga na klabu ya Rc Lens ya nchini Ufaransa, Hapo ndipo Hojlund atatambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa klabu hiyo.HojlundMshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Denmark ataweza kuungana na wachezaji wengine kadhaa ambao walipata nafasi ya kutambulishwa mbele ya mashabiki wa klabu hiyo katika dimba la Old Trafford kama Casemiro, pamoja na Raphael Varane.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Atalanta alifanikiwa kukamilisha vipimo vyake vya afya mapema jana pamoja na kusaini mkataba wa miaka mitano klabuni hapo ambapo sasa atasubiriwa kutambulishwa kesho.HojlundKlabu ya Man United katika vitu ambavyo wanajivunia kuvifanya katika usajili msimu huu ni kuhakikisha wanampata mshambuliaji ndani ya klabu hiyo ambaye ni Rasmus Hojlund ambaye wengi wanaamini atafanya makubwa ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe