Hojlund Kufanya Vipimo vya Afya Leo

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United Rasmus Hojlund amefika nchini Uingereza katika jiji la Manchester kwajili ya kufanya vipimo vya afya na kutangazwa rasmi.

Mshambuliaji Hojlund ambaye dili lake lilikamilika siku ya jumamosi usiku anaelezwa kufika jijini Manchester ambapo atafanya vipimo vya afya baadae na baada ya hapo atatangazwa kama mchezaji mpya wa klabu hiyo.hojlundManchester United sasa wanafanikiwa kupata mshambuliaji ambaye wamekua wakimuwinda kwakua klabu hiyo imekua ina tatizo la mshambulia wa mwisho hivo kumpata mchezaji huyo ni jambo zuri kwa klabu hiyo.

Man United wametoa kiwango kikubwa cha pesa kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 tu ambapo watu wengi wameonekana kupinga, Lakini wengine wameeleza kua mchezaji huyo ana uwezo mkubwa na umri wake ni mdogo hivo atakua klabuni hapo kwa muda mrefu.hojlundMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Denmark Hojlund alikuja kua chaguo la kwanza la kocha Ten Hag baada ya kuonekana dili litakua gumu kwa Harry Kane, Hivo ni wazi ni mchezaji ambae amekua chaguo la kocha na ana nafasi kubwa ya kufanya.

 

Acha ujumbe