Manchester City Walimtaka Balde

Taarifa zinaeleza kua mabingwa wa soka kutoka nchini Uingereza klabu ya Manchester City walikua wanamtaka beki kinda wa kushoto wa klabu ya Barcelona Alejandro Balde.

Manchester City walikua wanafuatilia kwa karibu mwenendo wa beki huyo kijana ndani ya timu hiyo kabla hajapewa mkataba mpya wa kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Camp Nou.manchester cityKlabu ya Barcelona wako kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumpa mkataba wa kudumu beki huyo mwenye umri wa miaka 19 ambao unaelezwa utakua wa miaka mitano hivo utamalizika mwaka 2028.

Klabu ya Manchester City ilikua inataka kufanya ujanja fulani juu ya Alejandro Balde ambaye alikua anamaliza mkataba wake, Lakini Barcelona walielewa mapema na sasa wanakaribia kumpa mkataba wa muda mrefu mchezaji huyo.manchester cityBeki Alejandro Balde amekua kwenye kiwango bora sana tangu alilpopata nafasi ndani ya kikosi cha wakubwa cha Barcelona akitokea timu ya vijana wa klabu hiyo, Huku ikimfanya kufikia mpaka hatua ya kugombea tuzo ya mchezaji bora kijana chini ya miaka 21.

Acha ujumbe