Manchester City na Nunes Kila Kitu Safi

Klabu ya Manchester City imefanikiwa kumalizana  na klabu ya Wolverhampton kwajili ya kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ureno Matheus Nunes.

Manchester City ambao walikua wanamuwinda kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno n maslahi binafsi baina ya mchezaji na City yalishafikiwa, Huku kilichokua kinasubiriwa ni makubaliano baina ya vilabu ambapo tayari yameshafikiwa.manchester cityKlabu ya Man City ilihitaji kutafuta kiungo  mwingine sokoni kwajili ya kukosekana kwa kiungo wake tegemezi Kevin de Bruyne ambae atakua nje ya uwanja kwa muda kidogo wakati huohuo walimuuza kiungo Ilkay Gundogan kuelekea Barcelona.

Matheus Nunes amekua akionesha ubora mkubwa sana ndani ya klabu ya Wolverhampton tangu ajiunge nao akitokea klabu ya Sporting Lisbon ya nchini kwao Ureno na kuwavutia Man City kuhitaji huduma yake.manchester cityManchester City sasa watakua Matheus Nunes, Rodri, Matteo Kovacic, John Stones, na Kalvin Philips kwenye eneo la kati ambao watakua wakitumika zaidi kwenye eneo hilo na baadae watajumuika na Kevin de Bruyne ambaye anauguza majeraha yake.

 

Acha ujumbe