Klabu ya Chelsea imehamishia nguvu kwa mchezaji kinda wa klabu Manchester City ambaye anacheza nafasi ya kiungo wa ushambuliaji anayejulikana kama Cole Palmer.
Klabu ya Chelsea mpaka sasa inaripotiwa kufanya mazungumzo na Manchester City kwajili ya kuhakikisha wanapata saini ya mchezaji huyo raia wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 tu.Matajiri hao kutoka jiji la London wapo sokoni bado kuhakikisha wanaijenga timu hiyo zaidi na zaidi ili kuirudisha kwenye makali yake ambayo imekua nayo miaka kadhaa iliyopita ambapo kwasasa inaonekana wameshuka kwenye ubora wao.
Taarifa zinaeleza kua Manchester City wamepiga chini kiasi cha paundi milioni 35 ambacho The Blues wamekipeleka kama ofa yao ya kwanza kwajili ya kinda Cole Palmer huku City wakisisitiza kua wanahitaji angalua paundi milioni 45 kwajili ya kumpata mchezaji huyo.Klabu ya Chelsea bado inafanya mazungumzo na Manchester City ili kuhakikisha wanakamilisha dili la mchezaji huyo, Kwani dirisha la usajili limebakiza siku mbili kutokea leo ili kufungw ahivo vilabu vinahitaji kuhakikisha wanapata saini zao mapema kabla siku hazijaisha.